KISONGO ACADEMIC COLLEGE

         KAC SECONDARY SCHOOL

      ARUSHA, TANZANIA

  

                    

  

                      

 

EMAIL:

STAFF/STUDENTS

  Students affairs:

Activites and Events

 

College Co-oparation:

Partnership and Sponsorship. 

 

 

 

 

 A WORD FROM

Board Chairman

 

 Partnership

 

Subjects

 

Contacts

 

How to join

 

construction for future

 

General

informations

 

Professional Training

 

Celebrations

 

Student leaders

 

Form one-2008

 

Form two-2008

 

Form three-2008

 

Staff members

 

JOINING INSTRUCTIONS

               2009

 

2009

School calender

 

 Family Day

2009

 

 

 

    

 

KAC JOINING INSTRUCTIONS

 


 

                  

MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE MWAKA 2009

 

Kwa niaba ya wanajumuiya wote wa shule na kwa niaba yangu binafsi nakupongeza kwa nia yako ya kujiunga na KisongoAcademic College kwa masomo ya Sekondari kwa kipindi cha miaka minne kuanzia tarehe 12/01/2009. Kama utafanikiwa kuchaguliwa na kujiunga nasi basi maagizo yafuatayo yatakueleza mambo muhimu kama:

 

1.0            Kufika shuleni:

1.1    Unatakiwa kuripoti shuleni tarehe 11/01/2009 bila kukosa , kwa wanafunzi wa bweni ni tarehe 10/01/2009.

1.2   Shule yetu ipo kilomita 13 kutoka mjini Arusha.Ufikapo stendi ya mabasi Arusha ulizia mabasi yaendayo Kisongo stendi unapaswa kumkumbusha akushushie kisongo stendi ,hapo utaona kibao kinachokuelekeza njia ya miguu ya kufika KISONGOACADEMICCOLLEGE, nauli ni T.sh 500 kutoka mjini.

1.3   Ikiwa unaikubali nafasi hii itakubidi kujaza fomu ya ahadi mwanafunzi Mzazi /Mlezi (SP-22) iliyoambatanishwa na kurudisha shuleni mapema. Kisha ulipe ada inayotakiwa kabla ya kuanza masomo. ADA IKISHALIPWA HAIRUDISHWI WALA HAIWEZEKANI KUHAMISHIWA KWA MWANAFUNZI MWINGINE.

1.4   Unatakiwa kuripoti shuleni kwa muda usiozidi wiki moja (Siku 7)Kuanzia tarehe ya kufungaua shule iliyotajwa hapo juu.Baada ya muda wa kuripoti shuleni kupita nafasi yako itatolewa kwa mwanafunzi mwingine.

 

2.0 Mihula

2.1 Mihula ya mwaka 2009.

Shule itakuwa na mihula mitatu kwa mwaka 2009

(i)                Muhula wa kwanza 2009 utaanza tarehe 12/01/2009 hadi tarehe 10/04/2009

(ii)              Muhula wa pili utaanza tarehe 20/04/2009 hadi 20/07/2009

(iii)            Muhula wa tatu utaanza tarehe 24/08/2009 hadi 11/12/2010

 

2.2   Mapumziko ya shule 2009

            (i)Siku zote za sikukuu zinazotambulika KITAIFA

2.3   Likizo za wanafunzi

            (i)Tarehe 10/04/2009 hadi 19/04/2009

            (ii)Tarehe 21/07/2009 hadi 23/08/2009

           (iii)Tarehe 10/12/2009 hadi 15/01/2010

 

3.0              ADA

     3.1 Wanafunzi wa  Bweni:-(KIKE)

Ada kwa mwaka ni         Tshs 530,000/=(Laki tano thalathini)

Muhula I: 2009             Tshs 220,000/=(Laki mbili na ishirini)

Muhula wa II: 2009      Tshs 160,000/=(Laki na sitini)

              Muhula wa III: 2009              Tshs 150,000/=(Laki na hamsini)

 

 

          Wanafunzi wa Bweni:-(KIUME)      Tshs  585,000/=

                         Muhula I: 2009                  Tshs 230,000/=

                         Muhula II.2009                 Tshs 180,000/=

                         Muhula III.2009               Tshs 175,000/=

         

  Sare za wasichana;

              Skati na Shati                Tsh. 24 ,000/=

              Sweta, Skafu,Tai,na soksi.   Tsh. 20,000/=

              Shamba Dress                Tsh. 10,000/=

              Michezo                       Tsh. 10,000/=

                   Jumla                                       T.sh. 64,000/=     

 

              Sare za wavulana:

              Suruali na shati                 Tsh. 24,000/=

              Sweta ,Skafu,Tai,na Soksi     Tsh. 20,000/=

              Sare za michezo                Tsh. 10,000/=

                Jumla                         Tsh.  54,000/=

                

              Mchango wa chakula;          Tsh.90,000/= KWA MWAKA

                                                                    Tshs. 30.000 kwa muhula

 

  

                                  KUANZIA MWAKA 2009 SHULE ITAPOKEA

WANAFUNZI WANANE (8) TU WA KIUME.

 

3.2 Wanafunzi wa kutwa:- (KIKE +KIUME)

 

SAMAHANI KUANZIA 2008  SHULE HAIPOKEI

TENA WANAFUNZI WA KUTWA.

 

3.3 Ada ya tahadhari(caution money)                      

Tshs 10,000/= Italipwa na kila mwanafunzi mara tu atakaporipoti shule na kiasi hiki kitarudishwa pale mwanafunzi atakapomaliza shule na kuwa amerudisha kila kitu cha shule.

3.4 Kinga ya vitabu Tshs 15,000/= Italipwa na wanafunzi wote nahii itarudishwa kwa mwanafunzi anapomaliza shule akiwa hana tatizo lolote na maktaba ya shule.

 

4.0            Ulipaji wa Ada:

Mzazi/Mlezi unashauriwa usilete fedha taslimu za ada shuleni. Ada ya shule  ilipiwe  kupitia Benki kama ifuatavyo:-

4.1   Kwa wale Wazazi/Walezi walioko Arusha Tafadhali lipa Kenya Commercial

4.2  Bank (T) Ltd iliyoko Arusha karibu na Kanisa la kiinjili la kilutheri mjini kati akaunti namba No.0221700181 Wale wa Dar es Salaam walipie  Kenya Commercial

4.3  Bank (T) Ltd uhuru road. Wale wa Mwanza walipie  Kenya Commercial

Bank (T) Ltd Mwanza co-operative union building. Pia kumbuka kuandika jina la mwanafunzi na namba yake ya shule;

4.4  Wazazi/Walezi wenye wanafunzi wa bweni wanashauriwa kuwapa watoto wao fedha kiasi za matumizi kama kununua sabuni,kalamu,dawa ya meno n.k.Wanafunzi wote wanashauriwa kuweka fedha zao za matumizi katika Ofisi ya Msarifu wa shule. Ni marufuku mwanafunzi kuweka fedha zake za matumizi bwenini.

 

5.0            Vitambulisho/Nembo

5.1   Kila mwanafunzi anapaswa kuwakilisha Tshs 2000/= kwa ajili ya kitambulisho cha uanafunzi.

5.2  Aidha ni lazima apigwe picha za passport size akiwa amevaa sare ya shule kwa ajili ya kumbukumbu za Ofisi.Picha hizo zitapigwa bure shuleni.

5.3  Pia kila mwanafunzi alipie nembi tatu (3) kwa ajili ya mashati ya shule pamoja na tai ya shule. Zote ni kwa Tshs 2000/=

  

7.0            Chakula

Chakula kitatolewa kwa wanafunzi wote , na chakula kikuu kitakuwa ugali, wali, makande na maharagwe kama kuna mabadiliko, basi ratiba ya chakula  itatolewa siku za jumatatu, kwa wiki yenye mabadiliko. Hali itakoporuhusu matunda ya msimu yatatolewa wakati wa chakula cha mchana au jioni.

  

8.0  Tovuti – Website.(www.kisongocollege.com)

Tovuti ya shule itakuwa ni chombo muhimu kwa kuitangaza shule, kutoa elimu, matangazo na maelekezo mengine muhimu ya shule.Kila mwanajumuiya wa shule atapata anuani binafsi ya –email katika tovuti hiyo.

 

9.0            Vifaa vya  darasani:

-Daftari kubwa zisizopungua 12 na calculata ndogo na vifaa vya hisabati;

-Kalamu za wino za kutosha na rula na vifaa vingine  muhimu.

 

10.0 Kuhudhuria Masomo:

Kila mwanafunzi anatakiwa kuhudhuria vipindi vya masomo yote yanayotolewa shuleni na kufanya mazoezi darasani na mitihani yote.Wanafunzi watakaoshwindwa kufuata sharti hili watarudishwa nyumbani.

 

11.0       Mahitaji/maelezo binafsi

11.1 Mavazi nadhifu na ya heshima yanayoendana na hadhi ya mwanafunzi wa sekondari,shule inayo sare rasmi ambayo hushonwa hapa shuleni.

                 Sare ya michezo:- wavulana – Bukta rangi ya bluu na T-shirt.Wasichana kigauni na bukta (P.T shorts)rangi ya bluu na T – shirt.Wote raba au viatu vya michezo na socks (Stockings)  rangi ya bluu.

11.2     Kwa wanafunzi wa bweni wanahitaji vazi la baada ya shule nalo hushonwa shuleni. ZINGATIA:Nguo za shule zisizo rasmi ni marufuku shuleni, kwa siku yoyote na wakati wowote,Epuka usumbufu usilete nguo hizo kabisa.

11.3     Viatu vyeusi vya kudumbukiza kwa wasichana na wavulana viatu vyeusi pia

11.4     Vifaa vya kulalia:Godoro la kawaida futi 3 urefu na kina inchi 4 Shuka 2 na chandarua cha kujikinga na mbu pamoja na blanketi kumbuka kuwa Arusha ni baridi majira ya jioni.

11.5     Vifaa vya chakula:Sahani kijiko na kikombe, na kikombe cha chai tafadhali siyo vya plastiki.La sivyo mwanao aje na kiasi cha Tsh.3500 ili vyombo hivyo avipate hapa shuleni.

11.6      Picha passport size 3 zitapigwa shuleni bure.

11.7      Vifaa vya kazi za kuboresha mazingira: ndoo 1 ya ujazo wa lita 20, jembe,slesha.

11.8     Kamusi ya ki-ngereza,[Oxford Dictionary],na ya Ki-swahili, ukipata na ya ki-faranza ni  Vyema sana.

          11.9  Rimu nzima ya kartasi nyeupe ya [Top Kopie -A4].

  12.0 Afya

            12.1 Unalazimika kupimwa na daktari katika hospital yoyote ya   Serikali       utokako

Kuthibitisha afya yako ya kumudu masomo haya.Nimeambatanisha fomu   (MED/CERT -21) ya kupimwa utakayoiwasilisha shuleni wakati wa kuripoti.

            12.2 Shule haitio chakula maalum (Special diet) kabisa.

            12.3 Shule itatoa matibabu ya huduma ya kwanza matatizo yote ya dharura katika  Zahanati ya P.A.G na Seliani zote za Kisongo na wazazi wataarifiwa ili kuchangia.

 

  13.0 Tahadhari

13.1 Uje na sanduku imara  kwa ajili ya kuhifadhi nguo na mali zako nyingine kwa      wanafunzi wa bweni.

13.2 Huruhusiwi kuja shuleni na vitu vya dhamani kubwa mfano;Simu ya mkononi fedha nyingi n.k

13.3 Uje na anuani kamili ya mzazi./mlezi wako.Iwapo unaye ndugu karibu na shuleni utoe taarifa mapema.

13.4 Uje na fomu hii ukiwa umeambatanisha (i)cheti halisi (Original) cha shule ya msingi.

13.5 Usije shuleni bila cheti hicho kwani hautasajiliwa kamwe.

13.6 Shule ina kanuni na sheria ambazo unapaswa kuzielewa na kuzifuata zimeambatanishwa na fomu hii.

13.7 Kama unakubaliana na maelezo yaliyomo kwenye taarifa hii , na sheria za shule kuanzia 12.1 – 12.25. Jaza fomu iliyoambatanishwa na maagizo haya kisha uiridishe shuleni;Itachukuliwa kuwa umeikataa nafasi ya kujiunga na shule hii uliyopewa usipokuja nayo.

 

14.Baadhi ya sheria za shule,

14.1 Kila mwanafunzi ni lazima awe mahali anapotakiwa bila kuchelewa kwa ujumla.                                                                                                    .

14.3 Kila mwanafunzi ni lazima afanye kazi kwa akili, maarifa, bidii na kujituma kwa uwezo wa ke wote.

14.4 Kila mwanafunzi ni lazima aheshimu na kutunza mali yake mwenyewe, mali ya shule mali ya jamii.

14.5 Hairuhusu kwenda katika nyumba za wafanyakazi isipokuwa kwa kibali maalumu cha mwalimu wa zamu

14.6 Ni marufuku kwa mwanafunzi wa jinsia ya kike kupatikana na mimba kwa kipindi chote watakachokuwa masomoni.Na .halikadhalika ni marufuku kwa mwanafunzi wa jinsia ya kike kuingia katika bweni la wanafunzi wa kiume.

14.7 Ni marufuku kwa mwanafunzi wa jinsia ya kike kupatikana na mimba kwa kipindi chote watakachokuwa masomoni.Na hivyo  ni marufuku mwanafunzi wa jinsia ya kiume kuhusika na kumpatia mimba mwanafunzi wa jinsia ya kike.Likitokea hilo waatafukuzwa shule na pia jambo hili litakabidhiwa vyombo dola

14.8 Ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote kuingia kwenye kilabu cha pombe,hoteli zenye vyumba vya kulala wageni/nyumba ya kulala wageni na baa.Ni marufuku kushiriki kileo chochote wala kuvuta sigara ya aina yeyote ile ikiwa ni pamoja na madawa ya kulevya.

14.9 Ni marufuku kukaribisha wageni na kuzungumza nao bila kibali cha mwalimu wa zamu au mlezi kwa siku za masomo isipoluwa siku za jumamosi jumapili na siku za sikukuu kuanzia 3:00 hadi 9:00 mchana  kibali cha mwalimu wa zamu.

14.10 Ni marufuku kupika na/au kupeleka chakula bwenini.

14.11 Ni marufuku kufanya vikao au mikutano ya aina yeyote ile bila kupata kibali cha Mkuu wa.shule.Matatizo yote yatafuata ngazi zilizowekwa na shule kuanzia serikali ya wanafunzi walimu wa zamumwalimu wa mabweni,maadili n.k

12 Ni marufuku kuendesha midahalo,malumbano ya kisiasa na mikutano ya kidini isiyo na kibali ndani au karibu na eneo la shule au mipaka ya shule, na pia ni marufuku kuwasiliana na vyombo vya habari bila kibali cha mkuu wa shule.

14.13 Ni marufuku kuanzisha, kuzuia na kueneza habari za kupotosha watu ambazo huwezi kuthibitisha ukweli wake.

14.14 Ni marufuku kumpotezea mwanafunzi mwenzako wakati kwa kumshirikisha,kumshawishi au kumlazimisha kutenda jambo linalokatazwa shuleni.

14.15 Ni marufuku kupatikana na kosa la wizi.

14.16 Ni marufuku kujihusisha na ugomvi wa aina yeyote ile hii ni pamoja na kupigana au kumpiga mwanafunzi mwenzako au kumtishia usalama wake kwa namna yeyote ile au kumdhalilisha kijinsia.

14.17 Taarifa ya msiba ni lazima itumwe kwa mkuu wa shule,utaruhusiwa kushiriki katika msiba iwapo aliyefariki dunia ni baba au mama mzazi au ndugu wa kuzaliwa tumbi moja.

14.18 Hakuna ruhusa mwanafunzi kumiliki simu ya mkononi akiwa katika enio lolote la shule.

14.19 Ni lazima kushirikiana na uongozi wan a viongozi wote wa serikali ya wanafunzi na pia kuonyesha ,moyo wa kujituma katika shughuli mbalimbali za kujenga shule na taifa letu kwa ujumla.

14.20 Pamoja na kutii na kufuata kanuni hizo,ni lazima kila mwanafunzi kuheshimu sheria zote za kitaifa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

14.21 Fedha za matumizi zikabidhiwe kwa mpokea fedha wa shule ofisini.

 Endapo wizi wa fedha utatokea shule haitahusika.

14.22 Ni lazima kuvaa sare wakati wote ukiwa shuleni au nje ya shule wakati wa kutoka au kuja shuleni.

14.23 Kutohudhuria masomo kwa jumla ya siku kumi na nne (14) au zaidi katika mwaka bila ya sababu maalumu kama kuugua hairuhusiwi.

14.24 Kumgomea mwalimu adhabu ni marufuku.

14.25 Mapambo kama Bangili,hereni,Mikufu ya shingoni.lipstic,kunyoa kipara,rangi za kucha, kuchoma nywele, kufuga kucha, kuvaa nguo fupi na nguo yinazoonyesha maumbile  nk haziruhusiwi shuleni.

                          

15.0 TOKA SHULENI

 15.1 Taswira ya KAC  ni wito kwa serikali,wananchi wote na wadau wote wa  maendeleo kuwekeza kwenye Elimu kwa akili, mali na muda.Kwa wanafunzi tumia muda vizuri ili ufikie tegemeo na maono (vision).

15.2 Pamoja na maagizo haya ya kujiunga na shule,tunaambatanisha fomu ya maelezo yako binafsi (SP-19) ambayo unatakiwa kujaza na kurudisha shuleni kabla ya siku ya mtihani wa kundi la mwisho wa kujiunga na shule ni tarehe.14 .January.2009.

15.2 Jumuiya  ya shule kwa ujumla inakutakia safari njema kuja shule na pia inakutakia maisha mema na ya mafanikio hapa  KisongoAcademicCollege.

                                            

 Eng. Calvin Marealle,

Mwenyekiti wa Bodi.

Bodi ya ushauri wa shule.

.

 

WEKEZA KWENYE ELIMU BORA:





             



 

 

 

 

 

 

 

Copyright ® 2008 Kisongo Academic College

          "WEKEZA  KWENYE   ELIMU BORA"

          "INVEST  IN  BETTER EDUCATION"

 

 P.O BOX 16181

 TEL: +255-733972397

 FAX:+255-732972397

 MOB:+255-755-464603/427267

 KISONGO VILLAGE

 LEKAMBA ROAD

 ARUSHA, TANZANIA.

Website:www.kisongocollege.com

Email:kac@kisongocollege.com